MAGUFULI AMEZURU MUHIMBILI

Raisi John Magufuli wa Tanzania afanya ziara ya kushtuza  Muhimbili toka aapishwe mnamo tarehe 5/11/2015.Ikumbukwe tu tarehe 6/11/2015 Mh.Raisi Magufuli alifanya ziara kama hiyo kwenye wizara ya fedha ambapo alikuta mapungufu mengi ikiwemo kukosekana kwa baadhi ya watumishi ambao walitakiwa kuwepo kwa siku hiyo. Ziara hii ya Mh. Raisi imekuwa ni moja ya ziara ambazo anazifanya ili kuona utendaji wa kazi katika sekta za umma.
PICHANI : Raisi John Magufuli akiangalia baadhi ya vyumba vya wagonjwa kwenye hospitali ya taifa Muhimbili.
Katika ziara hiyo Dkt  Magufuli alivunja bodi ya wakurugenzi ya hospitali ya taifa Muhimbili na kumuhamisha kazi aliyekuwa anakaimu kiti cha ukurugenzi wa hospitali hiyo Dkt Hussein Kidanto na kumteuwa Prof. Lawrence Mseru kukaimu nafasi hiyo kwa muda mpaka atakapotoa maelekezo zaidi.
PICHANI: Raisi akiwasili kwenye kitengo cha moi (kwa hisani ya Global publisher).

PICHANI : Raisi akisalimia baadhi ya wagonjwa

PICHANI : Raisi akiongea na mgonja Muhimbili

PICHANI : Raisi na mgonjwa Hospitali ya taifa

PICHANI : Raisi akimsalimu mgonjwa


Kama ilivyokuwa kawaida yake Mh Raisi alikutana na viongozi wa hospitali hiyo ya taifa Muhimbili na kuongozana nao kwenye kila eneo la hospitali hiyo kama atakavyo.Hata hiyo Raisi Magufuli kabla hajafanya ziara hiyo alipita  kumjulia hali mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi. Hellen Kijo Bisimba ambaye anapata matibabu yake kwenye hospitali hiyo baada ya kupata ajali barabara ya Ali Hassan Mwinyi akiwa yeye na watu watatu akiwemo mtoto mdogo, japokuwa wengine wote hali zao zinaendelea vizuri.
PICHANI : Raisi Magufuli akimjula hali Bi.Hellen Kijo(kitandani)
Aidha kwa upande wake Balozi Sefue pia amesema,   Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.

Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.

Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).

Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.

“Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao"
Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: