Mwanahabari nguli nchini Tanzania, hususani kwa habari zake za uchunguzi wa mambo tofauti ikiwemo siasa ya nchi yetu ya Tanzania ndugu Jenerali Ulimwengu amekabidhiwa tuzo ya mwanahabari mwenye mafanikio ya maisha na taasisi ya wanahabari EJAT (Excellence Journalism Award Tanzania) kutokana na kazi yake ya utafiti na utoaji habari kwa uhakika na ubora, tuzo hizo hizo zilizofana sana na kushiriki kwa wanahabari wa vyombo tofauti nchini zilifanyika 24/04/2015.
|
Pichani: Kwanza kushoto Mh. Galib Bilal, Pili kushoto Jenerali Ulimwengu, Pili Kulia Mke wa Jenerali Ulimwengu |
Tuzo hizo zilizopewa heshima ya kusimamiwa na mgeni rasmi makamu wa raisi Mh Galib Bilal, Aidha ndugu Ulimwengu alipata fursa ya kutoa dukuduku lake juu ya uongozi wa runinga ya taifa (TBC) kutokana na kuwekwa zaidi kwa manufaa ya chama kimoja tawala na sio kwa manufaa ya ya taifa kwa ujumla.
Waandishi kutoka gazeti la Mwananchi Mkinga Mkinga na Lucas Liganga waliibuka kuwa wanahabari bora wa mwaka huu wa 2015 na kukabidhiwa tuzo na kiasi cha milioni 3.8, wakiwa wote katika habari za uchunguzi.
|
Pichani: Kulia, Mkinga Mkinga akipokea tuzo ya mwandishi bira wa habari za uchunguzi |
|
Pichani: Makamu wa Rais Mh.Galib Bilal akimkabidhi Mkinga Mkinga cheki ya mfano ya kiasi cha milioni 3.8 pamoja na cheti cha uwanahabari bora mwaka 2015 |
|
Makamu wa Rais Mh.Galib Bilal akimkabidhi Lucas Liganga cheki ya mfano ya kiasi cha milioni 3.8 pamoja na cheti cha uwanahabari bora mwaka 2015 |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment