Katika Mkutano huo Raisi Magufuli amesema katika baraza hilo amejitahidi sana kubana baraza hilo kuwa dogo kwa manufaa ya watanzania, baraza hilo ambalo amesema litakuwa na mawaziri kumi na tisa(19) na wizara kumi na nane (18) na kuziweka baadhi ya wizara ambazo zilikuwa katika serikali iliyopita kwenye wizara moja.
Pia amesema kuchelewa kwake kutaja baraza hilo toka kipindi alichoapishwa ni kutokana na kubana matumizi ya fedha ambazo zingeweza kutumiwa kwenye baraza la mawaziri kwa kuwalipa mishahara na mengineyo na kusisitiza kuwa amejitahidi kuokoa zaidi ya billioni 2 zilizotengwa na ofisi ya serikali ya utumishi wa uma kwa ajili ya semina elekezi za mawaziri hao, na kuwaambia sasa hakutakuwa na semina elekezi badala yake waelekeze nguvu kusaidia wananchi.
0 comments:
Post a Comment