KIPIMO CHA MCI CHA REJEA TENA MUHIMBILI

Hospitali kuu ya Muhimbili nchini Tanzania,imesema kwamba mashine ya MRI imeanza kufanya kazi tena baada ya kurekebishwa.
Taarifa ya hospitali hiyo imesema kuwa kifaa hicho kimeanza kufanya kazi huku vifaa vyengine kikiwemo kile cha CT-Scan kikendelea kurekebishwa huku hospitali hiyo ikitarajiwa kutoa tamko lake kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi.
''Tunaomba radhi kwa matatizo waliyopata wagonjwa ambao walikuwa wanafanyiwa uchunguzi na kifaa hicho'',ilisema taarifa hiyo iliotiwa saini na mkuu wa mawasiliano bwana Aminiel Aligaesha. Urekebishaji wa kifaa hicho unafuatia ziara ya kushtukiza iliofanywa na rais John Pombe Magufuli siku ya Jumanne ambapo aligundua kwamba kifaa hicho cha CT-Scan kilikuwa hakifanyi kazi kwa kipindi cha miezi miwili swala linalowaweka wagonjwa katika mlolongo mrefu.
PICHANI : Mashine ya MCI iliyosemekana imeharibika
Rais Magufuli aliuagiza usimamizi wa hospitali hiyo kuhakikisha kwamba kifaa hicho kinarekebishwa kwa haraka iwezekanavyo.
Wakati wa ziara hiyo rais Magufuli alimuondoa kaimu mkurugenzi wa hospitali hiyo Dokta Hussein Kidanto na kuivunja bodi ya taasisi hiyo.
Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: