MKWASA AOMBA RADHI WATANZANIA

Kocha mkuu wa timu ya taifa stars,Charles Boniface Mkwasa ameongea na waandishi wa habari leo hii jijini Dar es salaam juu ya kutolewa kwa timu hiyo kwenye michuano ya kuwania kombe la dunia litakalofanyika Urusi mwaka 2018,Mkwasa alifanya hivyo kutoka na agizo la Raisi wa tff Jumanne Mlinzi alilotoa kwa kocha huyo kuongea na waandishi wa habari juu ya kipigo walichokipata dhidi ya timu ya Algeria.

Mkwasa amekiri uwezo wa timu ya Algeria kuwa ni kikubwa zaidi ya kiwango cha Taifa stars kwa sasa japokuwa jitihada alizozifanya zimeonekana na mabadiliko ya timu ya Taifa yanaonekana.

Aidha katika maongezi hayo na waandishi wa habari Mkwasa amewatupia lawama wachezaji wake kwa kutofanya yale aliyowaagiza kufanya uwanjani kisawasawa japokuwa amekubali kubeba mzigo wa lawama kutokana na matokeo ya sare 2-2 waliyoyapata hapa nyumbani, ikumbukwe Taifa stars na Algeria walitoka sare 2-2 kwenye mechi iliyochezeka Tanzania na kisha katika mechi ya marudiano iliyochezeka huko Algeria,Stars waliambulia kichapo kitakatifu cha magoli 7-0 na kufanya jumla ya magoli yote yaliyofungwa na Algeria kuwa 9-2.

“Tupo katika kipindi cha kujenga timu, tuna vijana wengi wanaochipukia, hivyo wanahitaji muda wa kucheza zaidi na kupata uzoefu, tuendelee kuwapa sapoti vijana hawa kwa ajili ya kujenga kikosi bora cha baadae” ameongeza Mkwasa.

Mkwasa amewaomba watanzania kuendelea kuwasapoti vijana, pamoja na matokeo mabaya dhidi ya Algeria, bado kuna nafasi ya kufanya vizuri katika michezo inayofuata ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2017.

Naye nahodha msaidizi wa Taifa Stars, John Bocco ameishukuru TFF kwa kuwapatia huduma bora za maandalizi na wakati wa michezo yao yote, amewashukru watanzania na vyombo vya habari kwa kuwapa sapoti na kuwaomba kuendelea kuwaunga mkono pindi wanapokua na majukumu ya kuiwakilisha nchi katika michuano mbalimbali.

“Matokeo ya juzi (dhidi ya Algeria) sisi wachezaji yametusikitisha, tulikua na malengo na mtazamo tofauti wa kupata ushindi, lakini katika mpira kuna matokeo matatu, tumepoteza mchezo huo kikubwa ni kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo na watanzania muendelea kutusapoti timu ya Taifa kama ambavyo mmekua mkifanya kwa sasa” alisema Bocco.




Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: