Ni mtanange uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na watanzania wengi kati ya timu ya taifa la Tanzania almaarufu kama "taifa stars" na Algeria timu inayoshikiria nafasi ya pili katika ubora wa soka Afrika,Matumaini ya watanzania wengi yalilenga ushindi kutokana na kujazwa na vijana wabichi na wabunifu pia wenye ari ya kuleta sifa kubwa ndani ya nchi hiyo huku timu hiyo ya stars ikiongozwa na kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa.
Kikosi cha kwanza kutoka kwa wenyeji(stars) kiliundwa na Ally Mustapha(G),Shomari Kapombe,Haji Mwinyi,Nadir Haroub(C),Kelvin Yondani,Himidi Mao,Thomas Ulimwengu,Mudhahir Yahya,Mbwana Samata,Elias Maguli na Faridi Musa. huku wachezaji wamiongeza ni Aishi Manula,Salim Mbonde,Mohamed Hussein,Saimon Msuva,John Bocco,Mrisho Ngassa,Malimi Busungu.
Kikosi cha kwanza kutoka kwa wageni Algeria kiliundwa na M'bolhi Rais(G),Mandi Issa,Ghouhlam Faouzi,Msloub Wald,Medjani Carl,Zeffane Mehdi,Guediora Aldane,Taider Saphir,Belfodil Isha,Slimani Islam,Mahrez Ryad na wa akiba ni Doukha Izeddine,Asselah Malik,Ziti Mohamed,Bensebaini Ramy,Abeid Mehdi,Bentaleb Nabil.
Mpambano ulianza kwa kasi sana na katika kipindi chote cha kwanza taifa stars walionekana kutawala mchezo kwa asilimia kubwa huku wakicheza mpira mzuri wa pasi, huku wachezaji Faridi Mussa na Elias Maguli wakikosa magoli mengine yakiwa ya wazi, lakini ilikuwa katika dk ya 43 ya kipindi cha kwanza cha mchezo ambapo Elias maguli aliwanyanyua watanzania kwa goli zuri kutoka pasi ya Thomas Ulimwengu,goli hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili pale mfungaji bora Afrika Mbwana Samatta alipopachika goli katika dakika ya 9 baada ya uzembe uliofanywa na mabeki wa Algeria na kumruhusu kuwakusanya kama kijiji na kutumbukiza mpira kunako nyavu zao.
Kocha wa stars, Charles Mkwasa alifanya mabadiliko kaika dakika ya 67 baada ya kuwatoa wachezaji Elias Maguli na Mudhahiri Yahya ili Mrisho Ngasa na S,Ndemla, endapo mabadiliko hayo kiufundi hayakuweza kuleta manufaa kwa kuwa katika dakika ya 71 na 74 mshambuliaji Slimani Islam alipachika magoli yote mawili kwa uzembe uliofanywa na mabeki wa stars.
mpaka naondoka uwanja wa taifa jijini Dar es salaam matokeo yalikuwa suluhu 2-2.
|
PICHANI : Kocha mkuu wa Timu ya Taifa stars Charles Mkwasa akiwatazama Algeria kwa umakini. |
|
PICHANI : Mashabiki wa stars wakionyesha mbwembwe za ushangiliaji. |
|
PICHANI : Wachezaji wakiingia uwanjani |
|
PICHANI : Kikosi cha kwanza Algeria |
|
PICHANI : Kocha wa Algeria |
|
PICHANI : Kikosi cha kwanza cha Taifa Stars |
|
PICHANI : Kikosi cha Akiba kutoka stars |
|
|
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment