MAKINDA : SINA NIA YA USPIKA TENA

Spika wa bunge la kumi Tanzania aliemaliza muda wake Bi. Anna Makinda, amekanusha taarifa za uvumi zilizoenea kuhusu kuwania tena nafasi hiyo kwa awamu hii ya tano ya uongozi wa Rais Magufuli,Makinda amesema hayo akiwa anaongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa hana nia yoyote ya kuchukua fomu na kuwania nafasi hiyo ya uspika wa bunge la 11.Alisema kuwa kwa taratibu za kugombea uspika  ni kwa muda wa miaka mitano na yeye ameshamaliza miaka yake mitano kwahiyo ni vyema kuacha wengine waongoze bunge.Amesema kisiasa amefikia miaka 40 sasa na ni vizuri ukifika miaka hiyo upumzike kisiasa.

Makinda pia amewapa sifa spika wa bunge la tisa ndugu Samuel Sitta na naibu spika wa bunge la 10 ndugu John Ndugai kuwa wanakila sifa za kushika nafasi hiyo kutokana na uzoefu wao lakini hata wale waliothubutu kuwania nafasi hiyo wanasifa za kuchuua kiti hicho.Akiwaelezea wanahabari amesema bunge la  kumi lmekuwa na changamoto nyingi kutokana na kujaa kwa damu changa ambao wameleta changamoto nyingi sana na kusababisha kubadili mzunguko wa bajeti na sheria ambapo haikuwahi kuwepo tangu miaka 50 ya uhuru."Ukipata wabunge wachangamfu kama waliopita hata kanuni utazijua tu kweli siwezi kulisahau bunge la 10" alisema Makinda.

Kati ya mbinu ambazo alizitumia kwenye bunge la kumi aliweka wabunge watundu ilikulichangamsha bunge.
PICHANI : Spika wa bunge la kumi Bi. Anna Makinda





Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: