MAGUFULI KUAPISHWA

Baada ya uteuzi wa Dkt John Pombe Magufuli kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya 5, kuanzia mwaka 2015-2020.Sasa imebaki kuapishwa rasmi kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Tanzania.

PICHANI: Raisi mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Dkt John Pombe Magufuli
Sherehe hizi za kuapishwa kwa mteule huyo wa kiti cha uraisi pamoja na makamu  zitafanyika katika kiwanja cha taifa kinachojulikana zaidi kama shamba la bibi mnamo tarehe 5/11/2015 jijini Dar es salaam.Dkt Magufuli aliteuliwa kwa kura za watanzania zenye uwiano wa zaidi ya asilimia 58 akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wote walioshiriki kinyang'anyiro hicho.

Mteule huyo atachukukua mikoba ya uongozi kutoka kwa mwenyekiti wake wa chama alichotoka ambaye pia ni Raisi wa awamu ya nne Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.Ambap pia imeelezwa kuwa ni demokrasia nzuri iliyooneshwa na Raisi huyo kwa kumuachia madaraka kwa amani bila vurugu, hii ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika zisizokuwa na tamaduni ya kufanya hivyo kama, Congo Drc,Burundi,Gabon na nyinginezo.
PICHANI: Raisi wa awamu ya Nne Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akipongezana na Raisi mteule wa awamu ya Tatu Dkt John Pombe Magufuli



Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: