BURUNDI HUENDA IKAWEKEWA ULINZI NA UMOJA WA MATAIFA

Umoja wa Mataifa unatafakari wazo la kutuma walinda amani nchini Burundi iwapo machafuko nchini humo yatazidi. 

Watu zaidi ya 200 tayari wameuawa na maelfu wengine kutoroka makwao tangu Aprili, Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba angewania urais wka muhula wa tatu.
Mnamo Jumatano, Rais Nkurunziza alipuuzilia mbali madai kwamba huenda kukatokea mauaji ya kimbari nchini humo na akawahimiza Warundi waungane.
Mwandishi wa wetu anayeangazia masuala ya usalama Afrika Joshua Neto anasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapiga kura baadaye Alhamisi kuidhinisha azimio la kukashifu machafuko Burundi.
PICHANI : Bendera ya Burundi

Kadhalika, mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali wanatarajiwa kutoa wito kwa UN na mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki kuchukua hatua.
Muungano wa Afrika tayari umekitaka kikosi cha polisi wa akiba cha kanda ya Afrika Mashariki kuwa tayari kutumwa Burundi iwapo hali itakuwa mbaya zaidi.
Hata hivyo, uamuzi wa kutuma wanajeshi nchini Burundi unafaa kufanywa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Milio ya risasi bado imekuwa ikisikika katika mitaa ya mji mkuu Bujumbura, huku raia wakishambuliwa mara kwa mara.
Nahodha wa timu ya kandanda ya rais Nkurunziza aliyetambuliwa kwa jina Jamal mwenyewe alinusurika kifo baada ya kupigwa risasi mara kadha miguuni Jumatano usiku.
Visa kama hivyo vinaipa serikali sababu zaidi za kuendelea na operesheni ya kusaka silaha katika ngome za wapinzani.




Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanasema serikali inaangazia tu wapinzani lakini haiangazii vitendo vya wanajeshi wake.
Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: