KUWAONA STARS NA ALGERIA NI KUANZIA SH 5000/= TU.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Jumamosi kati ya Tanzania dhidi ya Algeria utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam bei ya chini kuwa ni shilingi elfu tano (5,000) tu.

Tiketi za mchezo huo zitaanzwa kuuzwa siku ya ijumaa katika vituo mbalimbali vinavyotumiwa na TFF kuuzia tiketi, ambapo kiingilio kingine kitakua ni elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha elfu tano kikiwa ni kwa viti vya rangi ya Bluu, Kijani na rangi ya Machungwa.
Wakati huo huo kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhamininiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kurejea nyumbani leo mchana kwa shirika la ndege la Fastjet tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Algeria siku ya Jumamosi.
Stars iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya mazoezi kila siku katika uwanja wa Edenvale, ambapo mpaka sasa wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo wa Jumamosi.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana wake wapo vizuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali juu “wachezaji wamekua wakifanya mazoezi kwa nguvu na kuonyesha umakini mkubwa” alisema Mkwasa.

Mkwasa amewaomba watanzania na wadau wote wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti ya kuwashangilia vijana katika mchezo dhidi ya Algeria Jumamosi, kwani kutawafanya wachezaji kujisikia wapo nyumbani na kucheza kwa nguvu zaidi.
Wachezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu walioshinda kombe la Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa wiki na klabu yao ya TP Mazembe wanatarajiwa kuungana na wenzao kambini kesho jijini Dar ess alaam.
PICHANI : Stars wakiwa nchini Afrika ya kusini kuweka kambi dhidi ya mechi na Algeria hapo jumamosi
PICHANI : Kikosi cha kwanza cha Taifa stars kitakachopambana na timu ya Algeria siku ya jumamosi


Kwa upande wa pili, Msafara wa timu ya Taifa ya Algeria (The Desert Warriors) unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamis kwa ndege binafsi ya kukodi, ukiwa na jumla ya watu 65 wakiwamo wachezaji 24 tayari kwa mchezo wa Jumamosi Novemba 14 dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kocha mkuu wa timu hiyo Iitakayofikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Kempsinki, Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya kwa ajili ya kuikabili Tanzania.
Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili Alhamisi ni walinda mlango, Doukha Izeddine (JS Kabliye), M’bolhi Rais (Antalyaspor), Asselah Malik (CR Belouizdad), walinzi Zeffane Mehdi (Rennes), Medjani Carl (Trabzonspor), Ziti Mohamed (JS Kabliye), Mesbah Eddine (Sampordia), Bensebaini Ramy (Montpeller), Belkarou Hichem (Club African), Ghoulam Faouzi (Namples), Mandi Aissa (Reims).
Viungo ni Guedioura Adlane (Watford), Boudebouz Ryad (Montpeller), Taider Saphir (Bologna), Abeid Mehdi (Panathinacos), Bentaleb Nabil (Tottenham), Ghezzal Rachid (Lyon), Melsoub Walid (Lorient), Marhez Ryad (Leicester).
Washambuliaji  Benrhama Said (Nice), Sliman Islam (Sporting Lisbon), Belfodil Ishak (Beni Yas), Brahimi Yassine (FC Porto) na Bounedjah Baghdad (Etoile du Saleh).
PICHANI : Kikosi cha kwanza cha timu ya algeria kitakachopambana na Stars.
Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: