Akiapishwa katika hafla iliohudhuriwa na viongozi mbalimbali,wakiwemo marais kutoka mataifa ya Afrika mashariki na kusini, Magufuli ameapa kutimiza ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.
PICHANI: Raisi Magufuli akiwa ameshikilia ngao na mkuki kama njia ya ulinzi wa taifa hili kutoka kwa wazee wa jadi. |
PICHANI: Mh. Dkt J.P.Magufuli na Mh. Samia H.Sulhu |
PICHANI: Raisi John Pombe Magufuli akiapa mbele ya watanzania huku ameshika kitabu cha Biblia |
Magufuli ambaye sasa ni rais wa awamu ya tano nchini Tanzania vilevile amewataka viongozi wa upinzani nchini humo kukubali kushindwa na kushirikiana naye katika juhudi zake za kuimarisha maisha ya taifa hilo
Moja ya maneno #8 muhimu aliyoyasema kwenye hotuba yake Mh. Raisi Dkt John Pombe Magufuli ni haya yafuatayo;1.Naungana nanyi kumshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kutupitisha salama ktk kipindi cha Uchaguzi'.
2.Tumepokea dhamana ya kuiongoza TZ kwa nidhamu kubwa sana, tutafanya kazi kwa juhudi kubwa kutimiza ahadi.
3.Nawashukuru pia wenzetu wa Vyama vya Upinzani, mlikuwa washindani na sio wapinzani, nimejifunza mengi.
4.Uchaguzi umekwisha, tuungane kufanya kazi na kuweka pembeni itikadi na utofauti wa vyama vyetu.
5.Namshukuru Mzee Ali Hassan MWINYI kwa kuniongoza kwa busara zake.
6.Nawashukuru Mzee MKAPA na JK, sina cha kuwalipa, nitahakikisha natunza heshima yao kwa kufanya kazi nzuri.
7.Uchaguzi umekwisha, Rais ni John Pombe Magufuli.
8.Mimi ni Rais John Pombe MAGUFULI na Makamu ni Mama SAMIA, hapa kazi tu !! asanteni.
0 comments:
Post a Comment