TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MITIHANI YA ISLAMIC KNOWLEDGE

Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi nchini ,imetoa tamko la serikali juu ya dosari iliyotokea kwennye usahihishaji na utoaji wa majibu ya kidato cha sita mwaka 2012.

Tamko hilo limetolewa na waziri wa wizara hiyo mh. Shukuru Kawambwa kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Kawambwa alisema dosari hizo zimetokea hususani juu ya masahihisho na utoaji wa majibu wa mtihani wa Islamic knowledge wa mwaka 2012 ambapo alama zilizokokotolewa kwa mfumo wa kompyuta zilitofautiana.

Pia alisema baraza la elimu limekokotoa tena alama za mtihani huo na kurekebisha dosari hizo zilizotokea, na kuwasihi watanzania kutofanya maandamano ya aina yeyote kuhusu suala hili kwa kuwa limeshughulikiwa.
Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: