Kuongeza tija na ufanisi kwa wafanyakazi wa wizara ya fedha imetajwa kuwa ni nia kuu ya serikali kwa wafanyakazi hao
Hayo yameelezwa na waziri wa fedha nchini Dr William Mgimwa kwenye hotuba aliyoitoa ndani ya baraza la wafanyakazi hao lililofanyika Dar es salaam.
Dr Mgimwa alisema agizo la Mh Rais wa nchi ni kufanya baraza hilo kutoa na kujadili vitu ambavyo vinawatatiza kwa kuwa wizara ilfanikiwa kuzuia malipo ya wafanyakazi hewa takribani 9946 ambapo bilioni 5.1 zingelipwa kwa wafanyakazi hewa hao kwa mwezi
Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo ndugu Ramadhani Khijjah aliweka wazi changamoto zinazowakumba na kusema upatikanaji wa mikopo na utekelezaji wa uboreshaji wa mfumo wa fedha na mapato ya ndani imekuwa ikiwatatiza.
- Blogger Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment