SAKATA LA MGOMO WA MADAKTARI
-Sakata la mgomo wa madaktari nchini, leo limechukua sura mpya baada ya kipigo cha Mwenyekiti wa chama cha madaktari nchini Dkt Stephen ulimboka.Hayo yameonekana baada ya siku moja tu toka waziri mkuu wa nchi mh Mizengo Pinda baada yakusema kuwa atatoa tamko la serikali juu ya mgomo huo.
Mh Pinda aliitoa kauli hiyo baada ya msukumo mkubwa wa wabunge na wananchi juu ya kuharakisha tamko kutoka serikalini kuhusu mgomo huo, hata hivyo Mh Pinda alishindwa kutoa tamko hilo kama alivyoahidi na kuomba muda wa uchunguzi yakinifu juu ya wale waliohusika kwenye unyama wa kipigo cha Dkt Ulimboka.
Aidha kwa upande wake spika wa bunge mh Anna Makinda amesema kuwa serikali imesitisha kutoa tamko hilo kutokana na kuingiliwa na amri ya mahakama kutokana na suala hilo lipo chini ya mahakama kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment