DR. ULIMBOKA HOI
-BAADA YA MGOMO BARIDI WA TAKRIBA SIKU NNE(4) WA MADAKTARI NCHI NZIMA SASA ATHARI ZAJITOKEZA NDANI YA MADAKTARI WENYEWE KWANZA.
HAYO YAMEDHIHIRIKA BAADA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MADKTARI NCHINI DR. STEPHEN ULIMBOKA, KUKUTWA KWENYE KICHAKA HOI TAABANI BAADA YA KIPIGO KIKALI ALICHOKIPATA NJEE YA DAR ES SALAAM.
DR. ULIMBOKA ALISEMA USIKU WA KUMKIA JUZI KUNA WATU WASIOJULIKANA WALIMTEKA NA KUMPELEKA KUSIPOJULIKANA NA KUMPIGA, PICHA JUU KUSHOTO NI DR ULIMBOKA AKIWA KWENYE MOJA YA MAKONGAMANO YA MADAKTARI NA KULIA NI AKIWA KWENYE GARI BAADA YA KUKANDAMIZWA KIPIGO HIKO.
IKUMBUKWE KUWA MADAKTARI WAMEADHIMIA KUFANYA MGOMO HUO BAADA YA SERIKALI KUSHINDWA KULIPA MADAI YAO YA FEDHA HATA HIVYO MAHAKAMA YA KAZI ILITOA AMRI KWA MADAKTARI HAO KUTOGOMA KUTOKANA NA SERIKALI KUFUNGUA KESI YA MSINGI NDANI YA MAHAKAMA HIYO.
0 comments:
Post a Comment