CHELSEA YAZINDUKA ULAYA

Baada ya kipigo mfululizo kwenye ligi ya nyumbani ijukanayo zaidi kama "Premier League" na ligi ya mabigwa ulaya, timu ya wazee wa daraja la Stanford almaarufu kama Chelsea the blues, wamezinduka kwenye usingizi mzito wa vichapo  hivyo baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 2-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani Stanforbridge kutoka kwenye timu iliyojaa vijana wanaotafuta majina makubwa ulaya Dynamo Kyiv.

Chelsea iliyoingia uwanjani ikiwa na rekodi mbovu na hofu kubwa ya kupoteza mchezo wa kumi kiujumla, ilikuwa ni Aleksandar Dragovic kutoka Dynamo kwenye dakika ya 34 ya mchezo alipojifunga goli mwenyewe na kuwapa uongozi Chelsea mpaka pale alipokuja kukomboa goli hilo dakika 77 ya kipindi cha pili, na kufanya kuwa ushindani mzito kwa chelsea.

Hata hivyo kocha Mourinho alizidi kuchanganyikiwa pale refa alipokataa penati,  mpaka dakika ya 84 ndipo kiungo mkabaji kutoka Brazili  Willian aliwanyanyua washabiki wa Chelsea baada ya kupata pasi nzuri ya mpira wa adhabu kutoka kwa mbelgiji Harzad kama umbali wa miguu 25 hivi na kuwafungia goli la ushindi.Mpaka mechi hiyo inamalizika Chelsea walikuwa wanaongoza kwa goli 2-1.
PICHANI: Willian akishangilia baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Dynamo Kiev
Kwa ushindi huo sasa Chelsea imepanda mpaka nafasi ya pili kwenye kundi lao G wakiwafuata vinara wa kundi hilo Fc Porto waliowaacha pointi 3, na nyuma yao ni Kiev waliowaacha pointi 2.

VIKOSI:


Share on Google Plus

About Michael Neto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments: