Yusuf Manji amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans
Sports Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi,
kufuatia kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji,
mwenyekiti na makamu wake.
Akitangaza
matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond
Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John
Mkwawa amemtangaza Yusuf Manji kama mshindi wa nafasi ya uenyekiti
kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi
hiyo.Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga
aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u
makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron
Nyanda na George Manyama wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa
kamati ya Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa
kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilichopelekea kufanyika uchaguzi kwa
amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha
yoyote.Matokeo kamili ya wagombea ni:
Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%
- Blogger Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment